t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


ZIJUE HAKI ZAKO DHIDI YA JESHI LA POLISI

Katika kupinga ukatili wa polisi kwa wananchi inabidi wananchi kutambua haki zao za msingi dhidi ya polisi. Wananchi wamekuwa wakipata wakati mgumu pale ambapo wamekuwa wakijikuta mikononi mwa jeshi la polisi kama watuhumiwa. Wengi wamekuwa wakiokosa kutambua haki zao kisheria kwa kuwa ni elimu ambayo haitolewi katika mitaala yetu elimu katika shule za awali na watu wengine hawajabahatika kufika katika elimu za juu au kusomea sheria. Ufuatao ni muongozo wa awali kwa mtu ambaye hatambui kabisa mambo ya jinai na haki zake baada ya kujikuta mikononi mwa polisi kwa kuwa na hatia au kutokuwa na hatia kwa kuwa hilo huamuliwa mahakamani.

 

NINI MAANA YA JINAI? 

 Jinai ni kosa au makosa yanayofanywa na mtu au watu au taasisi kupitia watendaji wake, kinyume cha sheria za nchi au taratibu zilizoainisha makosa mbali mbali. Mfano wa makosa ya jinai ni kama kuua, wizi, ubakaji, uhaini na mengineyo.

 

Makosa hayo ya jinai husimamiwa na Utawala wa haki jinai. Ni mfumo wa usimamizi na utekelezaji wa sheria za nchi zinazohusu mwenendo wa makosa ya jinai. Hivyo kuna sheria inayoainisha kwa uwazi kwamba matendo flani yanapofanywa na watu kuwa ni jinai, pia  adhabu kwa matendo hayo ambayo ni makosa ya jinai. Shera hiyo ni Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 ya sheria za Tanzania (the Penal Code). Japo, kuna sheria nyingine mbalimbali zinazosimamia pia makosa ya jinai.

 

NINI TOFAUTI KATI YA JINAI NA MAKOSA YA MADAI? 

Tofauti kati ya Jinai na madai ni kwamba, kosa la jinai huhesabiwa ni kosa dhidi ya Jamhuri na madai ni lalamiko dhidi ya mtu binafsi, kampuni, taasisi au serikali kutokana na makubaliano fulani. Mfano wa kosa la madai ni kama kutolipa deni kwa mtu au taasisi kwa makubalino yalipangwa kati yao. 

 

WAJIBU WA JESHI LA POLISI NI NINI? 

Jeshi la Polisi kwa kiasi kikubwa linahusika katika maeneo ya ukamataji, uhifadhi wa watuhumiwa baada ya kukamatwa, mfumo wa kuwahoji watuhumiwa na upelelezi wa makosa ya jinai kwa ujumla, uaandaaji wa hati za mashitaka, uhifadhi, usafirishaji na uharibuji wa vidhibiti baada ya shauri kuhitimishwa au kabla ya hapo.

 

JE NI NAMNA GANI YA KUMKAMATA MTUHUMIWA? 

Kumkamata mtuhumiwa kunaweza kuwa kwa kutumia hati ya kumkamata au inaweza kufanyika bila kutumia hati ya kumkamata. Miongoni mwa watu ambao pia wanaweza kumkamata mtuhumiwa wa kosa la jinai ni pamoja na hakimu wa mahakama yoyote iliyowekwa kisheria, walinzi wa amani, yaani wajumbe wa nyumba kumi/mabalozi wa nyumba kumi na ofisa watendaji wa kata na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa.Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai”



NINI HAKI ZA MTUHUMIWA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI? 

Taratibu za kukamata hadi kuendesha mashitaka ya jinai husimamiwa na Sheria ya Mwenendo wa Makosa yaJinai ya Mwaka 1985 (Sura ya 20) na sheria nyingine kulingana na kosa la jinai. Haki za mtuhumiwa ni kama zifuatavyo;

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kuthaminiwa utu naheshima yake au kutoteswa pale anapotiwa nguvuni

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kuelezwa kosaalilotenda kabla ya kukamatwa.

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kupewa ushauri wakisheria.

  • Ana haki ya matibabu pale anapokuwa ameumizwaau anaumwa.

  • Ana haki ya chakula na malazi.

  • Ana haki ya kuwasiliana na ndugu zake.

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya mpakapale anapo hitaji huduma ya kuwakilishwa.

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kupata dhamana isipokuwa kwa makosa yasiyokuwa na dhamana.

  • kila mtuhumiwa ana haki ya kuyafahamu mashitaka yake.

  • kila mtuhumiwa anahesabiwa kuwa hana hatia hadihapo chombo chenye mamlaka (mahakama) ya kuzisikiliza tuhuma kitakapomsikiliza na kumuona na hatia dhidi ya kosa analotuhumiwa.

  • Kila mtuhumuwa atachukuliwa kuwa mwenye akili timamu katika sheria ya makosa ya jinai hadi hapovitakapothibitishwa vinginevyo mbele ya sheria.

 

NANI ANATOA MAMLAKA YA KUFANYA PEKUZI?  

Sheria inampa askari polisi mamlaka ya kufanya upekuzi katika nyumba za kuishi watu, ofisi, magari, vyombo vyovyote au maeneo yoyote kama atakuwa na sababu za msingi kufanya hivyo. Upekuzi pia unaweza kufanywa kwa mtu yaani katika mavazi yake au vitu alivyobeba.

 

JE UPI NI MUDA SAHIHI WA MTUHUMWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI? 

Kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa anatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya muda wa masaa 24 kama inawezekana, au apewe dhamana kama haitawezekana kufikishwa mahakamani ndani ya muda uliwekwa na sheria, isipokuwa tu kama kosa alilotuhumiwa nalo, halina dhamana.

 

Kwa kifupi hayo ndio mambo ya msingi ambayo mtuhumiwa na polisi wanatakiwa kuzingatia kuanzia mwanzo mtuhumiwa anapokamatwa mpaka hatua ya kufikishwa  mahakamani. Haki hizi Zinatakiwa kusiamiwa kwa ukamilifu na ikitokea mojawapo imevunjwa kwa makusudi bahati mbaya itahesabika ni uvunjifu wa sheria na mtuhumiwa atatakiwa kutoa madai ya haki hiyo mahakamani. 

 

#ActiveCitizens


download REPORT Posted on : 26 October, 2023