t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Mifumo Kandamizi Kwa Mtoto Wa Kike

Mfumo wa elimu haupaswi kuwa kandamizi kwa wanafunzi wa kike, serikali kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa elimu, inapaswa kutengeneza mfumo madhubuti ambao hautaweka vikwazo kwa mtoto wa kike kufikia malengo yake ya kupata elimu iliyo bora.

 

Wanafunzi waliopata ujauzito wana haki ya kupata elimu, kuwanyima elimu ni adhabu ya maisha yao yote hii ni kwa mama na mtoto wake. Hatupaswi kuwa na mfumo  kandamizi kama ilivyo sasa, mtoto wa kike anapopata mimba akiwa shuleni hili ni tatizo la jamii nzima sio peke yake, unatakiwa kumsaidia na kuweka mikakati ya kuondoa mianya inayosababisha ujauzito kwa watoto wadogo. Lakini pia tunatakiwa kuhakikisha   tunatengeneza  mazingira wezeshi yatakayowajenga kisaikolojia pamoja na kutengeneza njia bora zitakazo saidia watoto wa kike waliopata mimba kupata elimu  katika mfumo wa elimu iliyo rasmi.

 

Mtoto wa kike anapopata ujauzito hapaswi kujiuliza maswali juu ya mfumo wa elimu atakaopitia baada ya kujifungua bali anapaswa kutengenezewa mazingira wezeshi ili kuhakikisha kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuendelea na masomo yake kwa njia zinazokubalika na kutambulika kisheria.

 

Serikali inapaswa kuwarudisha wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali katika mfumo ulio rasmi na sio kuanzisha mifumo mengine ambayo ipo katika nje ya mfumo ulio rasmi. Hata hivyo serikali inapaswa kuhakikisha misaada mbalimbali inayotokana na sekta ya elimu ifanyiwe upembuzi yakinifu utakaowezesha wanafunzi kufaidika na mikopo hiyo kutoka mashirika mbalimbali duniani, kama Benki ya Dunia na Shririka la Fedha Duniani.

 

Mfumo kandamizi kwa mtoto wa kike una madhara mengi katika jamii likiwemo suala la kuongeza utegemezi katika familia, kuongezeka kwa wimbi la watoto wa mtaani, na kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali yanayochangiwa na madhara ya utandawazi, Hivyo basi ni muhimu kuondoa mifumo hii kandamizi ili kuwapatia watoto wa kike waendelee na masomo pasipo vikwazo vyovyote.

 

Utungaji wa sheria na sera mbalimbali za elimu uwe shirikishi, kwa kuhakikisha makundi yote yanayohusika katika sekta ya elimu yanashirikishwa na kutoa maoni yao pasipo ubaguzi au upendeleo na maoni hayo kufanyiwa kazi. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko katika jamii na kutengeneza misingi ya elimu iliyo bora kwa kizazi kijacho.

 

Jamii haipaswi kunyamaza mahala ambapo sheria na sera zinampoka mtoto wa kike fursa ya kupata elimu bali inapaswa kupiga kelele kwa kutoa njia mbadala za kuhakikisha kunakuwa na mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu nchini.

#ArudiShule #ElimuBilaUbaguzi


download REPORT Posted on : 21 June, 2022