Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.
The use of this website is subject to the following terms of use:
You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:
Wafadhili wamekua na mchango mkubwa sana kujitolea rasilimali kwa hali na mali kuhakikisha wanaboresha elimu nchini, wamekuwa wakitoa fedha ambazo zina kwenda moja kwa moja kujengea madarasa, vifaa vya elimu na miundombinu mingine ya elimu na hii yote inafanywa kwa manufaa ya mtoto wa kike. Wafadhili pia wanapaswa wafatilie utekelezaji wa mipango yao kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha malengo ya mtoto wa kike kupata elimu yanafanikishwa kwa kasi na kwa ubora katika mazingira sahihi.
Licha ya fedha nyingi kutolewa na wafadhili kutoka mashirika mbalimbali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya elimu kwa mtoto wa kike, lakini bado watoto wengi wa kike wanapata changamoto nyingi sana ili kupata elimu ukilinganisha na watoto wa kiume, baadhi wanasoma katika mazingira hatarishi yenye changamoto nyingi ambazo kwa namna nyingine zinawakwamisha kuendelea na masomo yao.
Serikali na jamii tunapaswa kuweka mazingira mazuri katika kupangilia mipango na matumizi ya pesa hizo za wafadhili, ili kuhakikisha fedha zote zinakwenda moja kwa moja katika masuala ya elimu hasa kuboresha mazingira ya watoto wa kike mashuleni, mtoto wa kike kupata elimu ni maendeleo yake pamoja na Taifa kwa ujumla, maendeleo ya mtoto wa kike yanawahamasisha zaidi wafadhili kujitoa kwa kasi zaidi katika suala zima la elimu, Fursa hii lazima iendane na udhibiti au thamani ya fedha katika matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa kwa watoto wa kike kwa kuhakikisha yanawanufaisha walengwa na wanapata elimu bora katika mazingira salama.
Jamii pia inatakiwa kuhamasisha serikali kuona haja ya kutozuia mirija ya aina yoyote inayopelekea mtoto wa kike kutoendelea na masomo yake, kwa kuondoa changamoto zikiwemo zakisera na sheria nchini ambayo kwa namna moja ama nyingine hazijatoa mwongozo wa namna gani mwanafunzi aliyepata ujauzito atarudi shule.
SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE YA MWAKA...
ZIJUE HAKI ZAKO DHIDI YA JESHI LA POLISI
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MH...
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Rip...
Ripoti Kuu Ya Mwaka Ya Mdhibiti Na Mkagu...
Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa H...