t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Historia ya wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule.

Baada ya kupata uhuru, Rais Julius K. Nyerere aliamini ili kuondokana na changamoto zinazokabili na kuchochea maendeleo elimu ndio chombo kikuu kinachoweza kutumika kukabiliana na changamoto hizo, zikiwemo umaskini, maradhi na ujinga. https://www.juliusnyerere.org/uploads/uamuzi_wa_busara.pdf 

 

Tulianzisha Sheria ya Elimu ya Taifa ya mwaka 1978 kupitia msukumo wa Nyerere wa elimu nchi nzima. Sheria hii haikujumuisha kifungu chochote chenye ubaguzi katika haki za Wanafunzi na wala haikusema kuwa ujauzito ni sababu halali za kuondolewa shule kabisa, Sheria hiyo ilimpa waziri mamlaka ya kuunda sera ambazo ‘Ataona yafaa kutekeleza’

 

Hatimaye mwaka 2002 serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Elimu na kuingiza kifungu kilichokuwa kinaruhusu kuondolewa shule kwa Mwanafunzi yoyote ambaye atakuwa amefanya makosa ya dhidi ya ukiukwaji wa maadili. Kifungu hiki cha sheria ndicho kilichopelekea waofisa mbalimbali katika ngazi ya elimu watoe tafsiri ya kuwa Kupata Ujauzito nalo ni kosa dhidi ya maadili, licha ya wao kutambua mabinti zaidi ya asilimia 36 walikuwa wakiolewa wakiwa chini ya miaka 14 kikiwa kiwango kikubwa kabisa katika nchi zote duniani, hivyo kufanya sheria hii kuwa kandamizi.

 

Mnamo mwaka 2009 Tanzania ilitunga Sheria ya Haki ya Mtoto, ikibainisha haki ya mtoto kuhudhuria shule, bila kujali jinsia au mazingira. Licha ya hayo, kufukuzwa kuliendelea kwa kasi ya rekodi. Inakadiria kuwa zaidi ya wasichana 8,000 huacha shule au kufukuzwa kwa ujauzito kila mwaka. https://www.bbc.com/swahili/habari-48677683  Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yanachukulia sera hii ya Tanzania kama ukiukaji wa moja kwa moja wa sheria zake za elimu na mikataba ya kimataifa waliyokubali kuidhinisha. 

 

Hatimaye mwaka 2017, Hayati Magufuli aliahidi kwamba hakuna mwanafunzi atakayepata ujauzito ambaye atamaliza masomo yake chini ya utawala  wake, akisema ni kinyume cha maadili kwa wasichana wadogo kufanya ngono.


download REPORT Posted on : 23 May, 2022