t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Changamoto wanazopitia wanafunzi wanapoelekea shuleni.

Jamii yetu ya kiafrika ina kumbwa na changamoto mbalimbali hususani watu wa vijijini, kwani kutokana na umbali mrefu kutoka shuleni wanafunzi wa kike wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali kama vile ubakaji. Tatizo hili la umbali linaweza kudhibitiwa endapo jamii kushirikiana na serikali kutengeneza makazi ya wanafunzi (Mabweni) maeneo ya jirani na shule na kuwawekea utaratibu maalum wa jinsi ya kuendeleza masomo yao. Hata hivyo vitendo hivi vinachagizwa zaidi na vijana ambao hawana elimu ya kutosha juu ya manufaa ya mtoto wa kike kupata elimu elimu bora. Hata hivyo jamii hizi zinapaswa kupata uelewa wa kutosha wa jinsi ya kumlinda mtoto wa kike na vitendo hivi vya uzalilishaji kwa mtoto wa kike.

Mtoto aliyebakwa huathirika kisaikolojia na pia kimwili, Ujauzito na magonjwa mbalimbali ya zinaa imekuwa changamoto kubwa kwa watoto wa kike katika jamii zetu. Hata hivyo mtoto aliyepata ujauzito anajisikia tofauti na kushindwa kuhimili shughuli zinazohusu elimu. Mfumo uliopo nchini kwa sasa ni kandamizi kwani unamruhusu mtoto wa kike kurudi shule kuendelea na masomo yake baada ya kujifungua Lakini hakuna sheria wala sera inayotoa mwongozo wa watoto wa kike kurudi shule hivyo basi inapelekea watoto wengi kushindwa kurudi shule baada ya kupata ujauzito na kutoendelea tena na masomo. Hata hivyo bado kuna utaratibu wa kufukuzwa kwa mtoto wa kike shule baada ya kupata ujauzito ambao unatekelezwa vizuri sana na wakuu wa shule.

Kumpigania mtoto wa kike ni jukumu la jamii nzima inaypohitaji maendeleo imara, kumpatia elimu mtoto wa kike ni chachu ya maendeleo katika jamii zetu na dunia kwa ujumla, na ili tufikie azma hii ni lazima tutatue changamoto zote anazokumbana nazo mwanafunzi wa kike akiwa anakwenda kupata haki yake ya msingi ya elimu.


download REPORT Posted on : 03 June, 2022